Rihanna na Drake wakikutana wanapotezeanaTunajua kuwa Riri na Drizzy walikuwa karibu sana na stori kubwa zikawa wawili hao wana date mpaka ikapelekea Drake kuzinguana na Chriss brown kwa ukaribu wake na Rihanna.

Mwanzo ilikuwa wanakataa kuwa hawafanyi lolote zaidi ya muziki na ushikaji, ila mwaka jana kwenye tuzo za MTV VMAs waliwahi ku kiss juu ya stage mbele ya camera na dunia nzima na hata kwenye shows zao na matamasha waliyowahi kupanda pamoja walikuwa wanahuh, kisses na Rihanna kutwerk kwa Drizzy!

Sasa baada ya Drake kuwa karibu na Jennifer Lopez na kudaiwa wana-date, Rihanna na Drake wakazinguana baada ya hapo ni mikausho mikali wakikutana, unaambiwa hawajapiga stori tena kuanzia hapo.

Hivi karibuni wamekutana kwenye tamasha la Coachella na kuminyiana vibaya, walipotezeana kila mtu na time zake.