Nay Wa Mitego Kuhusu Hali Ya Usalama Wake Kwa SasaRapa Nay wa mitego kwenye ukurasa wake wa Instagram jioni hii ameandika kuhusu kile alichokitaja kama kupungua kwa hali ya usalama wa maisha yake, Akionyesha kutilia mkazo Nay Wa Mitego ameandika kuwa kuna watu/mtu wanafikiria kumondoa kabisa kwenye ramani ya uso wa Dunia (kumuua).

"Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod🙏🏿
#Wapo
#Truth"

Ameandika Nay Wa Mitego: