Kwanini Kaka Wa Michael Jackson Alibadili Dini Na Kuwa Muislam?, Majibu Yako Hapa


 Kaka wa marehemu wa mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, Jermaine Jackson (Pichani) amefunguka kwanini aliamua kutoka kwenye Ukristo na kuwa Muislam,

Kwenye mahojiano na BBC, Jermaine amesema alivyowahi kwenda kwenye baadhi ya safari zake mwaka 1989 akiwa na dada yake anakumbuka walikutana na watoto ambao waliwapokea kwa ukarimu sana.

Jermaine amedai kupitia mazungumzo yake na watoto wale moja kati ya kitu alichogundua walitaka ajue mapema kama walikua ni Waislamu.
Jermaine amekaliliwa akisema "Ujasiri wa watoto wale ulinishitua" "Kisha walianza kuniambia kuhusu Uislamu, walinipatia mambo mengi , mengine niliyaona ni makubwa kuliko hata umri wao. Utamu wa maongezi yao ulitosha kunishawishi kwa kiasi gani watoto wale walikua wakijivunia kuwa Waislamu. Hivyo ndivyo nilijikuta naanza kuutamani Uislamu.

"Nilikaa na watoto wale kwa muda mfupi lakini waliniacha nikiwa bado ni mwenye maswali mengi kichwani kuhusu maisha ya Uislamu.Nilihisi kulikua na fikra nyingine kabisa kwenye akili yangu, Nikaanza kujipa moyo mwenyewe nikijiambia moyoni kwangu kama hakuna kilichotokea lakini sikuweza kuubadilisha ukweli kwamba moyoni wangu tayari ulishaanza kuwa na hisia za Uislamu" Amesema Jermaine.

Jermaine akiwa anaelezea kilichotokea baada ya kuwa Muislamu rasmi anasema "Nilijihisi muislamu mwenye aibu, nikajiona kama nimezaliwa upya, Jermaine amemeliza kwa kusema "Nikaanza kupata majibu ya maswali ambayo nilishindwa nikiwa Mkristo" . 

NB: TAARIFA HII HAIHUSIANI NA ISHARA ZOZOTE ZA UBAGUZI WA KIDINI