Kevin Gates ametupwa ndani miezi 30 kwa kosa hili lakini bado kufanya vizuri na mziki wake!


Rapper kutoka pande za Baton Rouge Marekani, Kevin Gates’ ametupwa jela miezi 30 kwa kosa la kuonekana ametumia bunduki kinyume na sheria,

Jamaa alionekana na kesi hiyo katika ofisi ya illinois, Jumatano ya April 26 kwa mujibu wa TMZ

Mwezi uliopita jamaa alikuwa na kesi ingine ya kumpiga shabiki wa kike usoni na kuchezea ndani kama miezi mitano hivi, baada ya kutoka inaonekana jamaa hakutokea mahakamani na kwa sasa msela wake unaweza kumfanya asote zaidi lupango.

Kevin Gates ni rapper aliyeimba ngoma ya 2 phones.
Jamaa amekuwa ndani tangu March 30 na kwa sasa atahamishiwa Illinois Department of Corrections.

Ukiachai mbali misala yake ya kutiwa ndani, bado anaendeleza career yake ya mziki, mapema mwezi huu aliachia ngoma yake What if na ameshirikishwa kwenye The Fate of The Furious Soundtrack ambayo ipo nafasi ya 10 billboard sasa hivi katika billboard 200.

Tazama interview ya Joh Makini