Joh Makini avunja ukimya kuhusu kumkopi Jay Z

Ni ukweli usiyojificha kuwa Joh Makini anamzimia Jay Z. Lakini rapper huyo amekana kuiga mistari kutoka kwa role model wake huyo.


Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihisi kuwa hitmaker huyo wa ‘Waya’ amekuwa akinakili baadhi ya mistari pamoja na kuiga flow kutoka kwa rapper huyo mkubwa duniani.
“Niambie mstari umesikia wa Jay Z nimetohoa, sijawahi hata kuchukua flow, kwasababu mimi ninarap maisha ya Sinoni, Daraja Mbili, Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn, Marekani,” Joh amekiambia kipindi cha Playlist cha Times FM.
Rapper huyo ameongeza, ana furahi akiwa anafananishwa na Jay Z kuliko angefananishwa na msanii mwingine.

Tazama interview nzima hapa.