IDRIS Sultan 'Sijawahi kukutana na Harmonize, alichukulia negative utani wangu'


Mshindi wa BBA 2014 na Comedian IDRIS Sultan mara nyingi amekuwa akiwatania mastaa wenzake kutupia pages zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter.

Mara nyingi idris anaweza kuona jambo na akalidandia na kuligeuza comedy kwenye mitandao, ila ilipofika kwa muimbaji wa Niambie, Harmonize idris aliambulia majibu ambayo hayakuwa poa kabisa kwake baada ya kumzingua Harmonize na ishu ya Harmorapa.

Idris alieleza Sababu ya kumtania Harmonize na kudai kuwa hawajahi hata kuonana muda wote huu! na kusema kuwa Harmonize alichukulia negative ishu hiyo, alichana mchongo huo kwenye kipindi cha The Playlist Times FM Jumamosi hii:

Tazama full interview hapo chini"