Dr Kingwangala ampa 5 za nguvu Ray CNaibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamisi Kigwangalla, amemtumia jumbe wa kumpongeza Mwimbaji wa kike Tanzania, Ray C na kuwaomba Wantanzania kumsapoti,

Ujumbe huo aliutuma kupitia paye yake ya instagram na kusema hivi:-

Na Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake, kama #BaloziWaWanawake na kama Daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada @rayctanzania, nimeguswa na wimbo wake wa #Unanimaliza, na nimeona nimuunge mkono kwa kuwaomba wadau wote ambao mmekuwa naye siku zote mfahamu kuwa sasa anahitaji support yetu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tumuunge mkono kwa dhati. Mungu atatujaalia kheir kwenye maisha yetu pia. Hakuna aliyekamilika. Sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka Na kwa hakika tunahitaji ‘a second chance’ kila siku za maisha yetu! Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka! Kila la kheir Ndg. Rehema Chalamila. With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing! #TeamBelieve #NjeYaBox #TanzaniaTuitakayo #MzeeWaField #SiasaNiVitendo #BaloziWaWanawake

 
 Na kwa upande wa Ray C nae alijibu hivi:-

” Heshima kwako Muheshimiwa, Nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja baba. Bless your soul Sir.”

Utakumbuka  March 24 Dr Kigwangalla alimsifia Diamond Platnumz kwa kuja na kuzindua Chibu Perfume na kumtaja mjasiriamali mzuri.


Tazama interview ya Diamond Platnumz hapa: