2 Chainz na Nicki Minaj Wainadi Ngoma YaoRapa mmarekani 2chainz ameutumia ukurasa wake wa Instagram kuuvunja ukimya kwa kuziongelea tetesi zinazoendelea kusambaa kuhusu Albamu yake ya nne “PrettyGirlsLikeTrapMusic”.

" I don't talk much but my song with her is goin to be a problem #prettygirlsliketrapmusic" Ameandika 2Chainz.

 2 Chainz amethibitisha kufanya ngoma pamoja na Nicki Minaj ambayo huenda ikatangulia ujio wa Albamu hiyo huku akidai kuwa ngoma hiyo ni tatizo miongoni mwa ngoma zote zitakazopatikana kwenye Albamu yake mpya.

 Nicki Minaj nae hakukalia kimya ishu hiyo kwani masaaa machache baada ya post ya 2 Chainz, Nick alitupia post yake na kuisindikiza na caption iliyozidi kuipamba ngoma hiyo.

“All Ima Say is Yikes” ameandika @nickiminaj.
Hii inakua mara ya kwanza kwa rapa hawa kukutana tangu walipofanya ngoma ya pamoja “Busy In Trap” mara ya mwisho mwaka 2012.