Mayweather aiweka gari yake Sokoni, Gari hizo ziko mbili tu Duniani.Floyd Mayweather ameamua kuiweka sokoni gari yake aina ya Koenigsegg CCXR Trevita, moja ya gari ambazo Duniani ziko mbili tu, Mayweather, Hakuna asiyefahamu kati ya magari ya kifahari ambayo anamiliki Floyd Mayweather, Stori ni kwamba Floyd ameamua kuiweka gari hiyo sokoni ya Koenigsegg CCXR Trevita ikiwa bado kali, Floyd Mayweather alinunua ndinga hiyo mwaka 2015 kwa mtonyo wa dola Milioni $4.8m. Licha ya kutotangazwa kwa bei ya ndinga hiyo, gari hiyo imehifaziwa huko jijini L.A ikisubiri mteja mwingine kuja kuichukua na yeye kuingia kwenye rekodi ya kibabe ya kumiliki gari hiyo. 

kwa sasa wanaomiliki Gari hizo ni wawili tu, ambao ni Hans Thomas Gross na Floyd Mayweather.