Ukarimu Na Umakini Wa Diamond Platnumz Ndivyo Vilimvutia Mrembo HuyuJina lake halisi ni Jessica Hearns model wa Marekani ambaye wiki hii anaendelea kujikusanyia mashabiki wa Afrika baada ya kuigiza kama Bi, Harusi kwenye Video "Marry You" ya Mbongoflava Diamond Platnumz aliyompa shavu Mmarekani Neyo.

alizaliwa pande za Detroit, Michigan State, Marekani,

Mwaka 2013 alihamia kwenye mji wa Las Vegas kwa ajili ya kujitafutia maisha yake ambako alianza kwa kufanya kazi kama waitress kwenye moja ya Cassino jijini humo.

 Akiwa Las Vegas  alifanikiwa kucheza "Reality Show" moja iliyokuwa ikionekana E! Network, ni Episodes 3  zilizompaisha na kumfanya mrembo huyo azitambue ndoto zake,
 Siku zote alitamani kuwa Model na Muigizaji mkubwa hivyo aliamua kukaza ili kuzifikia ndoto zake  alihamia jijini Los Angeles miezi saba iliyopita (yaani Mwezi August mwaka jana).
Tangu kuingia kwake Los Angels amefanikiwa kucheza kama Video Queen kwenye ngoma "In This World" ya mshikaji anaitwa Trevor Wesley pia ameshiriki kipengele kimoja kwenye "Whacked Out Sports"  moja kati ya shows maarufu Marekani.
Kwavile anapenda anchokifanya Jessica anasema kwenye moja ya Website zinazojihusisha na masuala ya uigizaji alikutana na tangazo lilikuwa likihitaji msichana mwenye asili ya kiafrika kwa ajili ya kuonekana kwenye video ya msanii mkubwa kutoka Afrika.

"Sikua namjua Diamond, Lakini idea ya video niliielewa nikatuma maombi, 
Wahusika walikuja kunipigia baadae na kuniambia kama walishapata msichana waliyekuwa wakimuhitaji lakini wakaniomba niwepo kwa dharula".  amesimulia Jessica.


"Nilifika eneo la tukio kabla ya muda hivyo nikajikuta mimi ni wa kwanza na bila kupoteza muda nikaingizwa chumba cha kubadilishia kisha nikafanyiwa Make-Up, Kila alieniona alinisifia wakijua mimi ndiye msichana niliestahili lakini niliwajibu hapana, Baadae Diamond Platnumz na timu yake walikuja chumba nilichokua na kwa baraka za Mungu walinipenda na kunichukua kama Bi. Harusi  kwenye wimbo huo.. 
Model Jessica amedai alichanganyikiwa baada ya zari hilo kumuangukia yeye.

 mpaka wamekamilisha Video hiyo  kitu ambacho anakumbuka ni ukarimu na umakini wa Diamond Platnumz na Timu yake (Yaani WCB WASAFI).

"Nakumbuka wakati tuna-shoot Diamond aliniambia nitakua maarufu kwenye nchi yenu mara baada ya video hii kuonekana" 


Kwenye sentensi nyingine Jessica H amesema Diamond Platnumz alihitaji shots nyingine nje ya Marekani hivyo walisafiri mpaka Afrika Kusini amabako walienda kukamilishia video nzima pande zile pale.

 "I am so grateful for all of the love I have been receiving from everyone in Africa and all over the world and I hope I can make it to see my biggest fans, friends and family in Tanzania soon!" Alimaliza kwa kuandika maneno hayo wakati tukipiga nae stori kwa njia ya mtandao.Diamond Platnumz - Marry You ft. Ne-Yo (Official Music Video)