Tazama Exclusive interview ya AY kwenye THE PLAYLIST Times FM

Linapofika swala la mshiko kwa AY ushikaji unakuwa pembeni, AY alidai chake baada ya kusikia kuna wimbo wake umetumika kwenye filamu ya Marehemu Steven Kanumba.


AY alimpigia simu Kanumba na Kanumba alikuwa kama anachukulia poa, AY alienda mbali zaidi na kwenda na mwanasheria ofisini kwao kudai chake, baada ya hapo hawakuongea kwa miaka kama mitatu hivi.


Ay alishangaa kuona stori hii mtangazaji wa kipindi cha THE PLAYLIST Times FM, Lil Ommy anayo na ameweza kumuliza swali kama hilo, tazama full interview.

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ya Muziki, AY alifanyiwa Surprise ambayo hatukuja kuisahau pale ambapo Lil Ommy alipomshangaza AY kwa kumchezea sauti za Dada yake akizungumzia kaka yake alivokuwa dogo, vitu alivyokuwa akipendelea mpaka mapenzi yake na muziki, Je hadi familia yake huwa anapenda kuwaficha vitu vyake?


AY alituchana kuwa kuuna collabo mwaka huu na Buster Rhymes, Wizkid, Ali Kiba na kuna collabo zingine kibao zipo ndani za Nameless, Fuse ODG na Project za AY na FA zitarudi anytime soon.


THE PLAYLIST ni Kila Jumamosi kuanzia Saa 6 hadi Saa 8 mchana na Lil Ommy kupitia 100.5 Times FM. 

VIDEO: