Kama Wewe Ni Shabiki Wa Trey Songz Hii Isikupite

\
Trey Songz ametangaza ujio wa Albamu yake m yake iliyopewa jina  Tremaine  inayotarajiwa kuingia sokoni 24/03/2017, Licha ya kuitangaza tarehe rasmi ya kuachiwa kwa Albamu hiyo ambayo itakua ni Albamu yake ya saba, Trigga hakuweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye ngoma hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa instagram mnyamwezi alipost moja ya cover zake huku Caption ikiwashawishi mashabiki zake kuweka order mapema. Trey hakutoa tu utambulisho wa albamu hiyo bali amewapa mashabiki  ofa ya wimbo "Nobody Else But You" (moja ya nyimbo zitakazokuwa kwenye Albamu hiyo).

Cheki Nayo Hapa:

 
Mbali na Albamu Trey songz ametangaza pia ujio wa series yake "Tremaine The Playboy" ambayo itakua ikiruka kupitia www.tremainetheplayboy.com kila siku za Alhamisi.. Kwenye website yake pia kuna T-shirt zenye maandishi yanayosomeka "Thanks God Its Tremaine" zitakazokuwa zikiuzwa online.