Kwanini Ni Don Jazzy Na Chura Ya Snura Mushi?
Big Boss Wa Mavinrecords Moja Kati Ya #RecordLabel Zinazofanya Poa Afrika Hapa Namzungumzia @donjazzy,Wikiendi iliyopita Aliwashangaza Baadhi Ya Watanzania Baada Ya Kupost Kipande Cha Video Kinachomuonyesha Akiimba Na Kuicheza #Chura Ya Mwanadada @snuramushi

 Kitendo ambacho kilionyesha kuwafurahisha Wapenzi Wa Bongoflava Hususan Mashabiki Wa Snura. Lakini Mapokeo ya mashabiki Yalikua Tofauti Kabisa Na Baadhi Ya Wanamuziki Wa Bongo,

Wapo Walioenda mbali zaidi wakidai hicho ni kitendo cha kawaida sana na kuwaponda waliochukulia kitendo hicho kama ni kitu kikubwa sana...

Wakati Nikitafakari Hayo Natengeneza Picha kuhusu Chura, Wimbo ambao Sina uhakika sana kama ulimlipa Snura Kutokana Na Misukosuko aliyokutana nayo Mara baada tu ya kuiachia #Video ya wimbo huo ikiwemo kufungiwa kwa video hiyo kuanzia mtandaoni mpaka Kwenye vituo vya televisheni
Kumbe licha ya kufungiwa wimbo huo ulishafanikiwa kupasua anga na kusogea Baadhi ya mataifa mengine. Wote tunaziona nguvu na jitihada wanazoziweka wasanii wetu wa bongo Kuhakikisha muziki wetu unaenda mbali,

 Bila shaka tunaijua level ya Snura. Ukiachana na Level yake Pia Chura sio #Hitsong kwa kipindi Hiki, Ninachojiuliza hapa kwanini Donjazzy na Chura?,  Kuna hitsongs ngapi Leo?, Unafikiri hazijafika Nigeria? Wapo wanamuziki wangapi Bongo Ambazo wametengeneza Connection #Nigeria Kwanini DONJAZZY hajajihusisha nao?

Kuna Wanamuziki wangapi wa Nigeria ambao walishafika Bongo, Kwanini sio wao lakini Donjazzy? Kwa Pamoja Kama Watanzania, tumpongeza @snuramushi Kwani Hicho Kidogo Alichofanya Donjazzy ni ishara kuwa sio Collabo tu za kimataifa zitakazotubeba Bali muziki wetu unajitangaza wenyewe hata tukifanya bila kushirikiana na mastaa wa nje.Cheki Don Jazzy akiimba na kucheza CHURA ya Snura: