EXCLUSIVE: Wengi walikuwa hawajui sauti ya kike 'intro' kwenye ngoma za Mabeste, ni Mke wake au?
Kama unafatilia kwa ukaribu sana utangundua kuwa karibuni kwenye kila wimbo wa Mabeste kuna sauti nzuri ya kike inasikika mwanzo wa ngoma zake kama intro, inayosema 'maabeestee'

Wengi walikuwa wanahisi sauti hiyo ni ya mke wake na rapper huyo, wengine walihisi ni Star wa kwenye filamu au muziki lakini hawakujua ni nani?

Sasa Sauti hiyo ni ya Vanessa Mdee, Mabeste alichana exclusive hiyo kwenye show ya THE PLAYLIST Times FM alipouliwa na mtangazaji wa show hiyo, 

Lil Ommy: hivi ile sauti ile yule mtoto anayesikika akisema maabeeste kwenye ngoma zako 'sexy voice' ni ya nani yule?

Mabeste: 'ile ni Sauti ya V, Vee Money, Vanessa Mdee, yeah nakumbuka miaka ya nyuma kipindi kile tunatafuta identity, unatafuta kitu gani ambayo utakuwa tofauti na artist wengine, aah mi nilikuja studio nikakuta Surprise tu, wakanimbia sikiliza hii, nikaona imekaa poa, tulifanya wakati nipo B Hitz. 

Mabeste full interview kwenye THE PLAYLIST: