Kama Ulikua Haujui Chochote Kuhusu Vevo, Huyu Diamond Platnumz Anakusanua

Diamond Platnumz anatajwa kuwa mtanzania mwenye watazamaji wengi zaidi kwenye chaneli yake ya youtube, Mara nyingi tumekua tukiona jinsi ambavyo video zake zimekua zikifanya vizuri mtandaoni ukilinganisha na za wasanii wengine. Februari 2,2017 Diamond Platnumz na uongozi wake wakishirikiana na Universal Music Group waliiachia video "Marry You" ambayo ndani Mmarekani Ne-yo amekula shavu, Tofauti na video zilipoita "Marry You" safari hii imeahiwa kwenye chaneli mpya ya mtandao wa Vevo.  Swali la kujiuliza kwanini Diamond Platnumz amekua mwanamuziki anaefanya vizuri youtube lakini hakuwahi kuwa na chaneli ya Vevo mapema?,  Swali lako analijibu hapa. "Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo... Nikawambia: "uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida..  Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo...na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo".....hivyo nikawambia: "siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida.... SABABU YA KUYASEMA HAYA: Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae... nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao..." kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh...🙏 -SIMBA #MALENGO" Ameandika Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram. Diamond Platnumz - Marry You ft. Ne-Yo