Tazama uzinduzi wa msimu mpya wa show ya The Playlist Times FM #toboakiburudani

Tarehe 14 January 2017 ulifayika uzinduzi wa msimu mpya wa show ya The Playlist uliokuwa na sura za mastaa kibao waliowahi kusikika kwenye show hiyo misimu iliyopita.Show ilikuwa LiVE kwenye redio ndani ya studio za 100.5 Times FM chini ya Presenter wake Lil Ommy huku baadhi ya mastaa wakijiachia kwa VIP treatment na Cocktail na Snacks wakati show inaenda hewani.

Show ya The Playlist inaruka kila Jumamosi kuanzia Saa 6 hadi Saa 8 mchana kupitia 100.5 Times FM na Presenter mnyamwezi Lil Ommy.


THE PLAYLIST imekuwa moja ya show kali za burudani kwa vijana inayoongoza kwa kusikilizwa Weekend, ni show ambayo inawashusha mastaa kibao kuchagua ngoma 5 wanazozikubali na kupiga nao mastori kibao kuhusu muziki, fashion na maisha yao kwa pande zote.


Kwenye show ya The Playlist unapata kuwasikia mastaa wakijiachia kwa muda mrefu zaidi kuzungumzia ishu zote zinazowahusu huku wakitaja list ya ngoma 5 wanazopenda. Utofauti mkubwa wa show hii ni ubunifu na ujanja wa maswali ambayo mastaa wanakutana nayo kwenye show hiyo kutoka kwa Presenter mkali Lil Ommy, The Baddest Boi aka Tambweeeeee.

Tazama UZINDUZI wa Show la THE PLAYLIST Times FM na Mastaa kibao, Hosted by LilOmmy: