Don Jazzy aimba na Kucheza ngoma ya Snura Chura


Producer mkali kutoka Africa, Nigeria Don Jazzy ameposti video clip kwenye account yake ya Instagram akiimba wimbo wa Snura kutoka TZ 'Chura' huku akicheza goma hilo.

Don Jazzy aliweka Caption ya Lol TZ did i get it right? #255 z#Chura


Hii sio mara yake ya kwanza Don Baba kudata na goma la Chura, aliwahi ku tweet kuhusu goma hilo long time.

pita pita zangu kwenye page ya Snura, sikuona Snura ame-respot wala nini, post yake ya mwisho inaonesha wiki mbili zilizopita.

Kiswahili ni lugha iliyopenya sana kupitia Muziki wa Bongo Fleva mpaka wasanii kama Yemi Alade aliitumia kwneye ngoma yake Asante (Nagode Remix) na katika clip hiyo Don Jazzy mtu mkubwa kwenye muziki Nigeria anaimba Kiswahili.